
Karibu kwenye mashamba yetu
Mashamba yetu yapo Vikonje ambapo ipo kwenye barabara inayoenda Morogoro,- kilomita 30 kutoka mjini Dodoma. Tunaonyesha mbinu endelevu, kama kilimo hifadhi, kilimo kwa njia ya Mungu, permaculture nk. kwenye hekari 60 (hekta 24).
Hivi sasa tumefuga wanyama karibu 100 na tumepanda zaidi ya miti 12,000.
Ili miti yetu ikuwe tunaboresha sana ardhi yetu. Tunafurahi kuwa na eneo letu la kuotesha miche na tunategemea kufungua duka letu la miti hivi karibuni. Watu wataweza kupata miche ya miti kutoka kwetu na kwa njia hii sisi tunasaidia kubadilisha mazingira ya Tanzania yawe kijani. Mifereji yetu inakinga maji wakati wa mvua, ili ardhi yetu iwe na maji mwaka mzima. Ardhi yetu inaongeza ubora mwaka hadi mwaka, kwa sababu mbinu zetu zinaboresha ardhi sana. Mavuno huongezeka kila mwaka.
Wakati idadi ya watu inaongezeka, mavuno yanapungua kila mwaka. Shida isipotatuliwa watu watakuwa na njaa kubwa sana. Huduma yetu ina mbinu nzuri sana kwa ajili ya kutatua shida hii. Sisi tunawafundisha watu, kutoka kwenye uhaba wa chakula, kwa kuwaelemisha wakulima na wakufunzi kulima kwa njia ya kilimo endelevu, kilimo hifadhi, kilimo kwa njia ya Mungu na permaculture.
Kwa sasa tuna wafanyakazi walioajiliwa 30 na wenginge wanapewa nafasi ya kusaidia kwenye huduma kama vibarua. Kwa njia hii tunasaidia jamii inayotuzunguka.
Tunafundisha semina mbalimbali kwa ajili ya kuelimisha wakufunzi na wakulima ili waelewe mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuendelea vizuri sana na mashamba yao na kuboresha mazingira yao.
Kupitia mashamba yetu ya maonyesho tunawaonyesha watu mifano ya kulinganisha mbinu mbalimbali. Tunalinganisha kilimo cha kienyeji, kilimo cha kisasa na kilimo kwa njia ya Mungu nk.
Huduma hii inaendeshwa na Kanisa la Anglikana Tanzania, Hilfe die ankommt, Care of Creation Inc. ikiwa inasaidiwa na watu wengi, ambao wanaona huduma hii ni jibu la maombi yao mengi sana kwa ajili ya Tanzania. Tangu mwanzo, huduma hii inafadhiliwa kupitia sadaka na michango ya watu binafsi. Lengo la muda mrefu ni kuona mashamba yetu yanajitegemea baada ya miaka.