NI SHIDA GANI ZA MSINGI AMBAZO ZINAPATA MAJIBU KWENYE HUDUMA YETU?
Huduma hii inalenga kuwaletea maelfu ya wakulima uhakika wa chakula. Wakati huohuo wanajifunza kutunza uumbaji wa Mungu kufuatana na mafundisho ya Biblia. Huduma yetu inawafundisha wakufunzi kutoka Tanzania yote na hata nchi nyingine za bara la Afrika, ili nao wafundisho mbinu hizo za kilimo endelevu na utunzaji wa uumbaji kwenye vyuo vya.
KINACHOHITAJIKA KWA JAMII
Wakati idadi ya watu inaongezeka haraka, mavuno kwenye mashamba yanapungua. Shida hiyo inatokea siyo Tanzania tu, bali kwenye karibu nchi zote za bara la Afrika. Kwa sababu hiyo kuna wakulima wengi mno ambao wanashindwa kujilisha vya kutosha kutoka kwenye mashamba yao, wakilazimika kula njaa au kupata lishe duni kwenye vyakula vyao. Hali hiyo inahatarisha afya ya, maendeleo ya uchumi kwa jumla, mafanikio ya watoto shuleni n.k.
HUDUMA HII INATOA MSAADA GANI WENYE UMUHIMU?
Bila msaada kwenye nyanja za elimu ya kilimo endelevu, usimamizi endelevu wa misitu pamoja na mbinu za kuvuna na kutunza maji ya mvua, hali ya maendeleo ya wakulima wa kawaida wa Tanzania itakuwa na changamoto kubwa. "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Huduma hii inalenga kwenye mabadiliko endelevu kutokana na mwingiliano wa mafundisho ya kiroho pamoja na ukufunzi wa kilimo endelevu. Mungu anawapenda watu na pia uumbaji wake bila kikomo.
Huduma ya Care of Creation Tanzania inapambana na changamoto hizo kwa njia zifuatazo:
• tunaendesha senta ya ukufunzi wa kilimo endelevu unaofuatana na mafundisho ya kiroho. Tunafundisha wakufunzi wengi ambao watawaongoza na kuwafundisha tena wengi wengine.
• Tunaendesha na kuendeleza shamba darasa lenye heka sitini kwa ajili ya majaribio na mafundisho ya mbinu mbalimbali za kilimo endelevu, k.m. kilimo kwa njia ya Mungu, permaculture, aquaponics, ufugaji endelevu n.k.
• tunashirikiana na wadau mbalimbali ndani ya Tanzania na nje
Kwa njia hiyo tunachangia kwenye mabadiliko endelevu ya kimwili na kiroho ya wakulima wa nchi ya Tanzania. Wakulima hawa watawezeshwa kuzalisha mazao ya kutosha kwenye mashamba yao na hata kuwalisha wenyeji wa miji ya Tanzania. Hivyo watamtukuza Mungu na kuona upendo wake mkuu kwa njia za pekee. Pia watajifunza jinsi ya kugawia upendo wake hata kwa uumbaji wake ili na uumbaji wake upate kuboreka kwa njia endelevu.