Historia

Baada ya kupokea wito mpya kutoka kwa Mungu kutumika katika eneo la utunzaji wa Uumbaji mnamo 2014, Alice na Martin waliwasiliana na Kanisa Anglikana nchini Tanzania, ambalo lilikuwa na heka 60 za ardhi ambazo hazikutumika karibu na chuo cha ualimu bila mtu yeyote kuzitunza, pamoja na maono ya kuwasaidia wakulima wadogo nchini Tanzania kutumia mbinu za kilimo zinazostahimili mabadiliko ya hali ya hewa kama vile Kilimo kwa Njia ya Mungu, mbinu za “permaculture”, kilimo cha miti nk. Kwa hivyo pamoja na shirika la ustawi la Austria "Hilfe die ankommt" na shirika la Amerika "Utunzaji wa Uumbaji" hati ya makubaliano iliundwa.

Walipofika kwenye shamba, lilikuwa limefunikwa na miba na lilikuwa na udongo mgumu sana, mpaka ilikuwa lazima kutumia sululu kuchimba!

Huduma ilianza na watanzania watatu na Alice na Martin, ambao walikusanya mbegu, kuotesha na kupanda miti, na polepole kusafisha eneo. Kwaya zilisaidiwa na kusafisha zaidi na kuchimba mifereji ya kuhifadhi maji.

Kama mvua nyingi zinanyesha bila kuingia ndani ya ardhi, maji mengi yanaondoka bure. Mbinu za kukinga maji ya mvua zinaongeza sana unyevu kwenye ardhi na kiasi cha maji ndani ya ardhi. Kutoka awali visima viwili tu vifupi, ambapo watu wangetafuta maji kwa kutumia vikombe vya kunywa, tumeweza kuchimba visima 14 vifupi zaidi ambavyo vimejaa maji kwa sababu ya kuvuna maji ya mvua.

Zaidi ya miti elfu ishirini imepandwa ardhini hadi sasa, karibu elfu sita ikiwa ni miti ya matunda. Mazao mengine ni k.m. mbaazi, muhogo, mtama, karanga, alizeti, mahindi, na mazao mengine kama vile fiwi na maboga ya asili.


Mfululizo wa Picha

kutoka 2017 hadi Leo

Hivi ndivyo eneo lilivyoonekana kabla huduma kuanza

Miti michache tu ilibaki kutoka kwenye misitu ya asili

Kikombe kilitumika kuchota maji kutoka kwenye kisima hiki

Wafanyakazi wetu walisafisha eneo la vichaka vya miba

Mitaro ya kukingia maji ya mvua ilipimwa…

Mitaro ya kukingia maji ya mvua ilipimwa…

5.jpg

…na kuchimbwa

6.jpg

Mifereji iliyokamilishwa inayofuatana na mwinuko

Miti ya kivuli ilipandwa na kukua kando ya barabara

Maelfu ya miti ilioteshwa

Mvua zilijaza mitaro yetu

Bwawa letu la kwanza lilijaa maji

Toroli la kutembeza kuku shambani wakati wa malisho

Mbuyu katika picha ya 2 baada ya kupata maji ya kutosha

Bustani nyuma ya nyumba baada ya mwaka wa kwanza

Uzalishaji wa mboga ulianza

Kundi letu la kwanza la kondoo lilifurahia malisho

14b.jpg

Eneo letu baada ya miaka miwili

Sehemu ya kuingilia mwaka wa tatu

 

Taarifa zaidi kuhusu maendeleo yetu utapata kwenye blogi yetu