Pilipili kichaa
Pilipili kichaa ni aina ya pilipili yenye kiwango kikubwa cha ukali.Kwa kawaida, pilipili hii hutumika kama kiungo cha chakula, lakini pia ina matumizi mengine katika kilimo na afya. Kuna faida nyingi za pilipili kichaa kwa matumizi ya kilimo endelevu pilipili kichaa hutumika kutengeneza dawa za asili za kuzuia wadudu waharibifu shambani. Mchanganyiko wa pilipili na maji unaweza kunyunyiziwa mimea ili kuzuia mashambulizi ya wadudu bila kuathiri mazingira.