Kuku

Eneo tunalofugia kuku lina ukubwa wa nusu heka, ambala tumezungushia uzio (fensi) na tumetengeza vibanda vidogo vidogo kwa ajili ya kulala na kutagia mayai kuku wetu, pia tuna
mabanda ya kulelea vifaranga.
Chakula cha kuku hatununi kilichochakatwa bali tuna nunua pumba tu na kuweza kutengeneza mchanganyiko wetu wenyewe, na ni chakula bora na chenye afya nzuri sana kwa kuku wetu.
Huu hapa ndo mchanganyiko wa chakula tunachowapatia kuku wetu.
i. Pumba ya mahindi
ii. Mbegu ya milonge
iii. Majani ya milusina
iv. Mafuta ya mlonge
Baada ya kuchanganya vitu hivyo hapo juu tunapata chakula cha kuku wetu.
Dawa
Kwa upande wa dawa pia tunatumia mara nyingi dawa za mime, na tunatumia mimea kama: Alovera,
na vitungu majani na hii ni angalao kila mara 1 kwa wiki
Na tunazingatia sana chanjo kwa kuku wetu na tunajitahidi sana kuwa chanja kila baada ya miezi 3.
Bila kusahau usafi wa mabanda yao kila wakati na kuhakikikisha kwamba wana pata maji muda wote
na kubadilisha maji katika vyombo vyao kila wakati.
Previous
Previous

Pilipili kichaa

Next
Next

Mfalme wa Amani