KILIMO KWA NJIA YA MUNGU

Mfumo wa kilimo kwa njia ya Mungu una sehemu kuu tatu ambazo ni.

1. Msingi wa kibiblia, huu unafundisha msimamo wa moyo unao takiwa kwa mtu kijiondolea

laana ya umasikini katika maisha yake.

2. Sehemu ya pili ni mbinu na hatua za kilimo kwa njiaya Mungu yenyewe.

3. Sehemu ya tatu ni nguzo za usimamizi bora na hii inahakikisha mafanikio katika kazi.

Sehemu zote hizi tatu zinaingiliana na kuunda mfumo wa kilimo kw njia ya Mungu.

FAIDA ZAKE

Hapa tutaonyesha faida kwa mfano.

Mwaka 2017 tuliandaa plot tatu zenye ukubwa sawa

Plot ya kwanza ni kilimo kwa njia ya mungu, Ploti ya pili ni ya kilimo kwa njia ya kisasa na Plot ya tatu ni ya kilimo cha kienyeji. Plot zote tatu zilipandwa zao la karanga kwa siku moja na ilikuwa kabla ya mvua kuanza kunyesha (mwezi wa 11) baadae mvua ikaanza kunyesha kwa muda na kusimama tena kwa kipindi kirefu. Na baada ya mvua kusimama kwa kipindi chote cha mwezi wa 12, ploti 2 ambazo ni kwa njia ya kisasa na ile ya kilimo kwa njia ya kienyeji karanga dhaifu sana na kukaribia kukauka kabisa, isipo kuwa katika ile plot ya kilimo kwa njia ya mungu ambayo karanga hazikupata shida ya jua kama zile plot nyingine 2. Ilipofika kipindi cha mavuno, mavuno yalikuwa kama ifuatavyo Plot ya kisasa debe 1 ya karanga, plot ya kienyeji tulipata ndoo 1 ya lita 10 na kwa ile plot ya kilimo kwa njia ya mungu tulivuna debe 3.

Kwani mavuno mengi katika plot ya kilimo kwa nji ya mungu?

Kwasababu katika ile plot ya kilimo kwa njia ya Mungu tunafunika na blanket ya Mungu ( matandazo) na hizo plot nyingine hazikufunikwa blanketi. Hapa chini nitaweka baadhi ya faida ya blanket ya Mungu. Hutunza unyevu(ubichi) katika ardhi yako, huboresha ardi na rutuba, huongeza wadudu wanao saidiakuboresha ardhi yako na mengine mengi. Kwa Elimu zaidi juu ya kilimo kwa njia ya Mungu basi karibu Care of creation Tanzania, karbu sana katika semina zetu ambazo zinatolewa kwa jamii yote bila kubagua dini, jinsia wala kabila. Karibu upate elimu mpya na kubadili maisha na mbinu mpya za kilimo kisicho na gharama kubwa zaidi ya gharama ya jembe tu la mkono.

Next
Next

Pilipili kichaa