Volunteers

Kila mwaka tunayo furaha ya kuwakaribisha watumishi wapya wa kujitolea kwenye shamba letu. Ni mara ngapi tumesikia sentensi: "Huu ni ulimwengu mwingine wa tofauti kubwa sana!"
Kwa kweli, mimea, wanyama na watu hapa shambani ni "tofauti" na yale uliyozoea au unayotarajia. Sio sisi tu kwenye shamba la majaribio na katika kituo cha mafunzo ambao ni "tofauti", wafanyakazi wetu wa kujitolea kutoka Ulaya ni "tofauti" na Watanzania wa hapa, pia. Hapa, kwa mfano, watu hapa hwajazoea kuangiliana machoni kwa muda mrefu, wakati huko Austria hiyo ni ishara ya heshima. Rangi yenye ngufu, vitambaa vya mapambo, vitu vya kumeremeta hupendwa hapa Tanzania, wakati huko Austria rangi na mapambo zimetulia sana. Tunaona tofauti hizi kama zawadi kubwa. Kwa njia hii, tamaduni mbili tofauti hupata fursa ya kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kufundishana kitu kipya na cha kutiana nguvu. Kusema kweli, mara nyingi tumesikia sentensi: "Nilibadilika sana wakati wa kujitolea hapa Tanzania". Tamaduni tofauti zina uwezo mkubwa wa kuzalisha nishati mpya kwa kila mmoja.
Wacha tusaidie kwamba hii ifanyike zaidi na kwamba nguvu nzuri, uponyaji, na amani huongezeka kwenye dunia yetu.
Previous
Previous

Lishe

Next
Next

Kila jambo lina wakati wake