Kila jambo lina wakati wake..!" - ukweli huo unaweza kuuona haswa wakati mimea inapokuwa. Ingawa unaweza kuchochea ukuaji kidogo kwa kutia mbolea n.k., lakini mimea bado inahitaji wakati wake. Nina rafiki mmoja mpendwa sana, aliyeniambia ya kwamba anahitaji muda wa kutosha kutazama wanyamapori. Kazi yake ni kusimamia wanyama wa porini maelfu, ili wawe salama. Ulimwengu wetu unaenda kasi sana na mara nyingi hakuna wakati wa mambo muhimu zaidi. Je unaonaje, mchakato bora unaolingana na sheria za Mungu kwa uumbaji ni kama ifuatavyo:
1. Tazama na chungulia
2. Fanya utafiti
3. Ujifunze,
4. Uruhusu jambo likomae.
Je, wewe unavyoishi unafuata hatua hizo au unasukuma mambo yaende mbele kwa speedi kubwa na kwa "LAZIMA"? Je, unasukumwa na pressure ya kila siku au unaongozwa na Muumbaji na sheria zake za uumbaji, ambazo zinakuhimiza kuchukua muda? Je, unachukua muda kuruhusu mambo yakue?
Leo ufurahi na kutazama na kujifunza zaidi kabla hujapiga hatua. Ujipatie msimamo wa kuwa "mwanafunzi" maisha yako yote!