Lo, Kenge!?

Ilikuwa Jumamosi mchana na ghafla nikasikia kuku wetu wakianza kukemea vibaya sana. Ni nini kilikuwa kikiendelea huko nje?  Kutazama nje ya dirisha kulinishangaza sana. Kenge mwenye urefu wa mita mbili aliwanyemelea kuku wetu. Lo! Alionekana kama mchanganyiko kati ya mamba na dinosaur.  Alikuwa mkubwa na alipendeza. Furaha na mshangao mwingi kwa Muumba ulitiririka ndani yangu. Ni zawadi la namna gani ya kwamba wanyama kama hao hupata kimbilio kwenye shamba letu. Tulitenganisha eneo la wanyama pori ambapo wanaweza kupata kimbilio na kujificha. Kila kitu ambacho Mungu aliumba ni kizuri sana. Tunaweza kuigundua tena na kusaidia kuikuza. Njia ni ya kusisimua na ya kushangaza na inahitaji furaha nyingi na ujasiri kuthubutu kujaribu kitu kipya.
Previous
Previous

Kila jambo lina wakati wake

Next
Next

Mtandao wa vyakula ardhini