Nyumba ya volunteers

IMG-20210408-WA0006.jpg

Leo napenda kutambulisha nyumba yetu kwako. Imekuwa kama nyumbani kwangu kwa miezi 8 iliyopita. Pamoja na wenzangu wengine watatu tuliojitolea tuliifanya nyumba hii kuwa nyumba yetu. Tulifanya kazi nyingi tangu tulipofika hapa. Tulibadilisha mabomba ya maji ya zamani, tukapaka rangi nyumba na vyumba kadhaa ndani (na tukachora picha nzuri ukutani), tukasafisha bustani yetu, tukapanda miti zaidi ya 60, tukafyeka nyasi mara nyingi, tukafanya mabadiliko katika nyumba ya umeme na kupaka rangi nyumba nzima ikawa nyekundu. Majirani zetu wanapenda rangi na kila mara hutabasamu wanapopita. Tulijenga pia mahali pazuri pa kupumzika juu ya nyumba yetu. Unapanda ngazi na kufurahia manzingira ya kiafrika. Wakati mzuri wa hii ni jua linapo chomoza na jua linapotua! Pia tulinunua chandarua kwa ajiri ya kupata nafasi ya kukaa usiku kule. Hivi karibuni tunataka kujenga jiko mpya na kukarabati bafuni yetu. Kwa jumla ni mahali pazuri kualika marafiki, wafanykazi wenzetu na wageni na kuwa na chakula cha pamoja na kufurahi.

Previous
Previous

Mashimo ya kupandia migomba

Next
Next

Wageni wa Jumapili ya Pasaka