Mashimo ya kupandia migomba

SAVE_20210420_155026.jpg

Kwenye eneo letu mvua zinanyesha tu kwa miezi sita hivi kwa mwaka. Kwa hiyo ni muhimu sana kukinga na kutumia maji haya ya mvua kadiri inavyowezekana. Mvua ikinyesha inaweza kunyesha kweli kweli! Hapo tunahitaji mbinu za kukinga maji na kuyalazimisha yaingie kwenye ardhi badala ya kuondoka bure tu. Mbinu tunazotumia ni mifereji ya kukingia maji, mabwawa na pia mashimo ya kupandia migomba.

Shimo la migomba ni shimo lenye upana wa mita mbili na kima cha mita moja hivi. Hilo shimo tunajaza na viozeo (kama makapi, mashudu, samadi, majani mabichi, miiba n.k.), tunafunika na matandazo ya majani au nyasi na kupandia migomba na mimea mingine. Mashimo haya tunachimba pale ambapo maji ya mvua yanakusanyika nu kuanza kutembea. Hivyo tunakinga maji haya na kutengeneza mfuko wa unyevunyevu ardhini ambao unapunguza mahitaji ya kumwagilia kiangazi. Viozeo na matandazo yanapunguza kuvuka kwa maji hewani, na pia vinarotubisha udongo vizuri sana.

Sehemu nyingine ambapo tunatumia mbinu hiyo ni kwenye maji taka ya mabafu na jikoni. Maji taka ya bafuni na jikoni yana sabuni nyingi na uchafu mwingine, kwa hiyo hayafai kwa umwagiliaji. Lakini yakiingia kwenye shimo lenye viozeo, sabuni na uchafu wote vinaozea humo ndani na maji yanatumika mara ya pili kunywesha mimea na mbogamboga.

Picha hiyo inaonyesha wazi ya kwamba migomba yetu inafurahia sana mbinu hii!

Previous
Previous

Impact Shedrack

Next
Next

Nyumba ya volunteers