Impact Shedrack

shedrack nzuriiii.jpeg

Bwana yesu asifiwe sana. Nawapenda wote katika Bwana. Nimezaliwa mwaka 1994 mkoani Dodoma. Mimi ni wa pili kuzaliwa katika familia yetu. Lakini kwenye familia tumebaki mimi na Baba kwa sababu ya kipindupindu. Hivyo basi wakati nikiwa mdogo niliishi na Bibi baada ya Mama kufariki. Ila baadaya kuwa kijana nikarudi kwa Baba.

Elimu yangu nilibahatika kusomeshwa na ufadhili kutoka nchi za Ulaya hii kutoka na hali yangu dhaifu ya uchumi na kuonekana kuwa na juhudi sana katika masomo ya shule ya msingi .Ufadhili ulinisomesha shule ya msingi hadi chuo. Kwa sasa nina taaluma ya ualimu kwa shule za msingi. Nimehitimu mafunzo ya ualimu mwaka 2016.

Baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu nimekaa nyumbani miaka 3 bila kupata kazi . Hivyo basi nikatuma maombi katika huduma ya Care of Creation Tanzania. Mungu ni mwema na wa huruma, akasikia kilio changu nikakubaliwa kuwa katika huduma ya Care of Creation Tanzania mwaka 2020. Japo kulitokea janga kubwa la corona ilibidi baadhi ya wafanyakazi tupumuzishwe kidogo.Baada ya hali kukaa vizuri tukarejeshwa katika huduma tena.

Huduma hii ina maana kubwa sana kwangu, jamii na kwa taifa zima.Kwa sababu imetuelimisha kulima kwa njia ya Mungu pia inatoa matokeo makubwa sana katika jamii na inaifanya nchi kuwa ya kijani kwa kipindi kirefu.

Hata pia huduma hii imeniongoza kwa kupitia mkono wa Mungu kutatua shida mbalimbali maendeleo ya familia kwani imenisaidai upatikanaji wa chakula, mavazi na malazi katika familia.

Natoa shukrani zangu za dhati kwenu, Mungu awabariki sana. (Yeremia 33:3)”Niite nami nitakuitikia nitakuonyesha mambo makubwa ,magumu usiyoyajua.”

Sh.D.Hwaiti

Previous
Previous

Mwalimu mpya

Next
Next

Mashimo ya kupandia migomba