Mwalimu mpya
Siku za hivi karibuni tumepata neema kubwa ya kuwa na chumba kipya cha kujifunzia kiswahili kwa wageni wanaokuja kutoka sehemu mbalimbali kujitolea kushiriki katika huduma yetu ya utunzaji wa uumbaji. Chumba ni kizuri na kina mabenji,viti na meza kwa ajili ya ujifunzaji. Pia kuna dirisha kubwa linaloingiza mwanga na hewa nzuri na ya kutosha. Kwa upande wa mwalimu tumebahatika kuwa na mwalimu mahiri na mzoefu mwenye taaluma ya ualimu ambaye amekuwa na mchango mkubwa sana katika kuwafundisha lugha ya kiswahili wageni kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Ni mwalimu mahiri kwani anafundisha kwa vitendo na kuwawezesha wageni kuituumia lugha ya kiswahili katika stadi zote nne za lugha ambazo ni kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika.Tangia chumba kipya cha kujifunzia kuanzishwa, mwalimu anafurahishwa na mwitikio wa wanafunzi kwani wamekuwa na uwezo wa kusikiliza na kuelewa maana,kuzungumza,kusoma na kuandika. Lengo kuu la kuanzisha darasa la lugha ya kiswahili kwa wageni ni kuwafundisha kanuni na taratibu zinazotawala sarufi ya lugha ya kiswahili kwa kuzingatia matawi manne ya sarufi ambayo ni matamshi,ya lugha ya kiswahili utwasaidia sana wageni kutumia lugha ya kiswahili katika mawasiliano ya kila siku katika huduma yetu ya utunzaji wa uumbaji. (mwandishi Kuyi Mabula)