Vigae vya nyumba ya mkutano
Kila asubuhi saa nne tunakutana sisi sote kwa ajili ya kuimba, kuomba, kusoma Biblia na kulitafakali neno. Tumefanya hivyo kwa miaka mitatu sasa katika nyumba yetu ya mkutano. Nyumba hiyo ni kubwa, ya mviringo na unajisikia kwamba uko kwenye mazingira matamu sana, kwa sababu hewa inaingia toka pande zote. Kwa sasa tumebarikiwa kupata ufadhili wa kutuwezesha kuweka vigae kwenye nyumba hiyo. Tunafurahia uzuri wa msonge wetu, maana kusafisha na kuing‘aarisha ni rahisi zaidi sasa. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa ajili ya msaada wa kifedha na tunaomba sana mtuombee ili tuweze kukutana kwenye nyumba hiyo kwa upendo na kukutana na Uzima wa Mungu kila siku tunapokutana kwenye nyumba yetu mpya inayong‘aa vizuri zaidi.