Mapya kutoka kwenye nyumba ya volunteers

Kitchen.jpeg

Mwezi wa nne na watano karibu mfululizo tulikuwa na matengenezo kwenye nyumba yetu. Tulianza na ujenzi wa jiko jipya Kabati za zamani za mbao ziliondolewa na kubadilishiwa na kuweka kabati za sementi. Halafu pampu ya maji ilikufa tukalazimika kwenda kisimani kwa siku nne kuchota maji ya kuoga na kupika. Baada ya pampu kutengenezwa tu, kulikuwa na shoti kwenye nyumba yetu ambayo iliharibika umeme wote. Lakini sasa, baada ya wiki tatu bila jiko zuri, siku nne bila maji kwenye nyumba na wiki moja bila umeme, tumefikia hali nzuri tena. Tunamshukuru na kumsifu Mungu kwa kutupa nguvu, uwezo na uvumilivu wa kutosha. Kabati mpya jikoni zinatufurahisha sana. Zile za zamani hazikuwa na nafasi ya kutosha, tena ilikuwa vigumu kufanya usafi vizuri. Jiko jipya lina nafasi ya kutosha kwa vyombo vyote na linasafishika kwa urahisi zaidi. Pia tunashukuru kwa pampu mpya ambayo inasaidia watu wengi chuoni na hata kwenye shamba letu. Kwa sababu ya shoti ile Volunteers wetu watatu Matthias, Danieli na Mattheo walilazimika kubadilisha nyaya zote kwenye nyumba. Ilianza ijumaa moja jioni, wakati tulipofurahia wikiende yenye utulivu. Ghafla umeme ukakatika. Kesho yake tukaweza angalau kutengeneza soketi moja kwa ajili ya kuchaji simu zetu. Ila vyakula vyote kwenye friji na friza tulihitaji kutumia haraka iwezekanavyo! Baada ya wiki moja yenye kazi nyingi umeme unafanya kazi tena. Ingawa shoti hii ilikuwa usumbufu, hata hivyo tunamshukuru Mungu kutulinda na mabaya zaidi, na pia kwa kutupa uwezo wa kutengeneza mfumo wote wa umeme vizuri.

Previous
Previous

Vigae vya nyumba ya mkutano

Next
Next

Kampeni ya Upandaji wa Miti