Impact Daudi

Daudi mbigili.jpeg

Mimi naitwa Daudi Mbijili Njani, ninawasalimu watu wote wapendwa katika Bwana Yesu Kristo wa Nazaleti mwana wa Mungu aliye hai. Mimi ni mzaliwa wa kijiji cha Vikonje B katika wilaya ya Dodoma mjini Mkoa wa Dodoma. Ninamshukuru Mungu sana kwa kuwa katika huduma hii ya kilimo kwa njia ya Mungu, yaani „Care of creation Tanzania“. Binafsi ninamshukuru Mungu sana baada ya kupata kibali cha kuingia huduma hii kilimo kwa njia ya Mungu nimeona ina manufaa na faida kubwa sana kwangu, kwa familia yangu, katika jamii na kwa taifa zima la Tanzania. Yafuatayo ni baadhi ya manufaa ya huduma hii ya Care of Creation Tanzania: Inatoa mazao makubwa katika eneo dogo, inarutubisha ardhi, inaponya ardhi kutoka hali ya nusu jangwa kuwa pa kijani. Hii ni kutokana na njia na mbinu mbalimbali zinazotolewa katika huduma hii. Mfano mmoja ni utumiaji wa blanketi ya Mungu (majani makavu) yanayowekwa chini ya miti au mazao mbalimbali yanayopandwa. Nimeona mkono wa Mungu ukitenda miujiza kila iitwayo leo. Kwanza baada ya kunikutanisha na watumishi wa Mungu ambao ni Alice Tlustos na Martin Tlustos, hii ilikuwa ni muujiza mojawapo kutokea kwangu, pia baada ya kukutanishwa na hawa watumishi wa Mungu nimejifunza kilimo hiki kwa kiwango bora, yaani kutumia vipimo na kufuata hatua kwa hatua katika kilimo kwa njia ya Mungu. Kwa kweli Mungu ana nguvu na mamlaka katika ulimwengu mzima. Pia nimejifunza kuwa na upendo wa Mungu na tumaini la kumtegemea Yeye, kuishi kwa imani, kutokuwa na chuki na watu wengine, kuwajali na kuwasaidia watu wenye hali yoyote. Haya ni matunda kupitia Meneja na Mkurugenzi. Haya ni machache kwa ufupi ujumbe wangu unatoka vitabu vifuatavyo. Mwanzo 1:11-12 na 2 Wakorintho 9:6-8. Asante sana, na Mungu awabariki.

Previous
Previous

Tunarudi nyumbani Austria

Next
Next

Vigae vya nyumba ya mkutano