Tunarudi nyumbani Austria
Sasa muda wa kuondoka kwa volonteers wetu umefika. Tunasikitika sana kuondoka kwenye mashamba ya kilimo kwa njia ya Mungu. Muda wa kukaa huko Tanzania ulikuwa ni muda mema sana. Tumejifunza mambo mengi mapya na mazuri sana. Tumejifunza kilimo hifadhi, lugha ya Kiswahili na mambo mengi ambayo yalikuwa mageni kwetu. Kila siku tulipata nafasi kuongea na wafanyakazi na kutumia maneno mapya tuliyojifunza. Kila mmoja wetu alikuwa na kazi nyingine ambapo aliweza kuonyesha utalaamu wake. Hii ilitufurahisha sana. Daniel alikuwa anajenga system ya aquaponics na alimfundisha mfanyakazi mmoja wa Tanzania kuiendeleza. Matthäus alisaidia kujenga fensi ya kuku na kuendeleza ufugaji endelevu kwa kuku wetu. Pia aliandika kitabu cha wananyama pori mbalimbali, wanaoishi kwenye mashamba yetu. Pia Matthäus akamfundisha Mtanzania mmoja kuendeleza ufugaji wa kuku. Matthias alitengeneza tovuti ya huduma yetu na kumfundisha mfanyakazi mmoja kuiendeleza. Pia mwwaka huo tuliboresha nyumba ya volonteers. Mwaka huu hatutausahau na ni wa maana sana kwetu. Tunamshukuru sana Mungu kwa ajili ya baraka hii na tunawatakia kila la heri na salaam tele kule Tanzania!
Daniel, Matthäus na Matthias