Miti inayobariki maisha yetu kwa jumla
Hapa kwenye mashamba yetu kila mwaka miti inatusaidia kupunguza upepo mkali na vimbunga. Pia miti inatupatia hewa safi na tunaona miti kwetu ni ishara ya amani na baraka. Ukiwa unatembea chini ya miti unajisikia vizuri sana na inafurahisha. Miti ni uhai kama miti haipo basi na uhai hautakuwepo. Miti imekuwa inatusaidia sana kwenye maisha yetu kwa faida nyingi, mbalimbali kulingana na aina ya miti. Miti inapunguza joto na hewa chafu ya kaboni ambayo imekuwa inaongezeka sana dunia, lakini pia ina faida nyingi zingine kama vile chakula, matunda, dawa na n.k. Tuzingatie sana maana ya miti ili tuishi maisha marefu sisi sote