Hekima ya mchungaji

IMG-20210615-WA0004-02.jpeg
Tunao kondoo 60 hivi kwenye mashamba yetu endelevu. Tuna wachungaji na mbwa wanaochunga kondoo hawa, ili wapate kula kwenye majani mazuri na wafurahie maisha yao. Mchungaji mmoja ana hekima sana. Siku moja nilimwuliza ya kwamba anaweza akaniambia nini ili nijifunze zaidi kwa
maisha yangu. Akasema hivi: “Kila asubuhi ninapofungua zizi na kutoka na kondoo wanafurahi sana,- maana wana njaa kubwa na wanapenda kupata chakula haraka. Tunapotoka sasa kondoo wanakimbilia majani ya njiani na wanaanza kula yasiyo bora sana. Ila mimi kama mchungaji wao, nimeona wamekula nini jana yake na ninajua watapata wapi majani bora yatakayowasaidia kiafya na hata kwa kunenepa. Kwa hiyo ni kazi sana kuwahamasisha waondoke kwenye majani yasiyo bora na kutembea mpaka pale ambapo mimi nimepachagua tangu awali. Mimi ni mrefu na ninaona mbali
zaidi kuliko wao. Tunapofika kwenye majani bora kondoo wakianza kula wanasahau majani yale yasiyofaa ya njiani na wanafurahia majani niliyoyachagulia.“ Vilevile Mungu anaelewa zaidi mahitaji yetu.

Previous
Previous

Huduma ya Ngamia

Next
Next

Tours kwenye mashamba yetu