Kwenye shamba letu kwa kilimo hifadhi tunaonyesha njia mbalimbali za ufugaji wa wanyama. Moja ya spishi za wanyama ambazo tungependa kuweka kwenye shamba letu hivi karibuni ni ngamia. Kwa nini ngamia? Unaweza kupanda ngamia na ni njia hifadhi ya usafirishaji. Lakini sio hayo tu – unajisikia kipekee sana ukiwa unapanda mnyama kama huyo. Hauketi kwenye "sanduku la chuma lililokufa" lakini juu ya kiumbe hai ambaye pia ana sifa zake. Unaweza pia kugusa manyoya, na unasikia mwendo wa ngamia unapokaa juu yake, na unavuta hewa safi ukiwa unasafiri naye. Ngamia inatoa faida ya ngozi, manyoya, nyama na maziwa yenye thamani sana. Nina uhakika ya kwamba, hupaswi kukosa kupanda ngamia. Ni tokeo la kipekee linalovutia saaana.