Ushuhuda wa Mwasembe

Zeugnis MA Mwasembe-02.jpeg
Mimi naitwa Wiliadi Halidi Mwasembe, nimetoka kijiji cha Luhanga kata ya Luhanga wilaya ya mbarali mkoa wa mbeya. Kwanza na mshukulu Mungu wa mbinguni kwa kunipa kibali cha kufika hapa nakujiunga na huduma hii ya care of creation Tanzania. Tangia mwaka 01-09-2017 ndipo niliingia katika huduma hii. Kwanza eneo hili lilikuwa vichaka tu pili kulikuwa hakuna nyumba, kulikuwa hakuna miti ilikuwa imekatwa kwa ajili ya kuchoma mkaa pia  ardhi ilikuwa haima rutuba na kulikuwa na visima vitatu ambavyo wananchi walichota maji. Navyo maji yalikauka yalikuwa ya foreni ndefu na mara nyingi wananchi walikosa maji. Hayo niliona mwenyewe sio kuambiwa wala kuhadithiwa.
Mimi ni mkulima toka nyumbani lakini nilipoingia katika huduma hii niliona ukulima wangu ni kupoteza nguvu tu. Nilikuwa nalima pakubwa lakini kipato kidogo. Kwanza nilitumia pilau au jembe la ng’ombe au trekta au jembe la mkono. Sikuweza kutumia mbolea kwa sababu ya gharama yake.
Tulipo anza mwaka wa 2017-01-septemba tulianza kuandaa viproti vitatu: kiproti kwa njia ya Mungu, kiproti kwa njia ya kisasa na kiproti kwa njia ya kienyeji. Kiprot kwa kilimo kwa njia ya Mungu tulipanda mahindi tukafunikia majani ambayo tunaita blanketi ya Mungu, kiproti ya kisasa hatukifunikia majani wala kitu chochote; ila vipimo ni sawa na kiproti cha kilimo kwa njia ya Mungu: Shimo hadi shimo sentimiter 60 urefu, na sentimiter 75 mstari hadi mstari. Kiproti cha kienyeji hicho hakima utalamu wowote. Vyote tulipanda siku moja na mwaka huo mvua ilinyesha kuanzia mwezi 11 ilisimama hadi mwezi wa 1 mwenzi wa kumi na mbili haikunyesha. Tulipanda pia karanga kwenye viproti vitatu. Cha ajabu mavuno Kiprot kwa njia ya Mungu tulipataa debe tatu, kiproti cha kisasa debe 2 na kiproti cha kienyeji debe 1 na nusu. Wakati huo wa kuanza kulima wakulima majirani walikataa kwamba hatuwezi kupata chochote. Kweli hata mimi mwenyewe sikuamini kwa sababu ardhi ilikuwa ngumu mno kuchimba mpaka tulihitaji kutumia sululu. Hayo kwangu yana maana sana. Na kupanda miti kwa njia ya Mungu kwa kuzingatia maelekezo ya mafundisho ya walimu wetu pia nayo miti lazima baada ya kupanda lazima uweke blanketi. Tena nimepata elimu ya kutosha ambayo inanitoa katika uhaba wa njaa hata kama mvua ndogo nina uhakika wa kupata.
Previous
Previous

Mnazi

Next
Next

Huduma ya Ngamia