Miezi michache iliyopita tulianza kujaribu kuotesha mbegu za minazi. Nyingi zimeshaanza kuota. Ili iote vizuri unatakiwa kufanya hatua zifuatazo: Kwanza unaweka nazi chini vizuri inakaa sawasawa upande ulio pana zaidi. Hatua ya pili ni kuweka mbegu vizuri katika usawa na kuchonga ganda laini ya nje upande wa mbele. Hatua ya tatu ni kuchimba shimo halafu unaweka mbolea kidogo na udongo kidogo juu ya mbolea ili mbegu inapoota mizizi isikutane moja kwa moja na sumu ya mbolea. Lakini unachimba shimo kina nusu ya mbegu. Halafu unaweka mbegu kwenye shimo na unafukia nusu mbegu inayoonekana juu kwa udongo. Hatua nyingine unaweka blanketi ya mungu (nyasi). Baada ya hapo unamwagilia na mwisho unaiombea iote vizuri na kukua vizuri. Kuanza kesho yake unamwagilia mara mbili kwa siku robo keni. Hapa kwetu Dodoma mbegu zinaota kuanzia miezi miwili hadi sita lakini maeneo mengine muda huu unaweza kuwa tofauti.