Kupanua eneo la bustani ya miti

SAVE_20210329_165332.jpg

Mwezi wa kumi mwaka uliopita tuliongeza eneo la bustani ya miti Tumegundua ya kwamba eneo hilo halitaweza kututosha, kwa sababu Mungu amepanga mambo makuu kwa ajili ya bustani hii! Kwa hiyo tumepanda miti ya kutoa kimvuli, ambayo pia inazaa matunda matamu sana. Pia tumeshazungusha eneo jipya na fensi ndogo. Mfanyakazi mmoja amepanda maua mazuri kulizunguka eneo letu. Mengine yameshachanua. Miti ya kimvuli nayo inaota vizuri, na tunamwomba Mungu itoe kimvuli haraka. Pale ampabo tayari kuna kimvuli tumeshaanza kuotesha miche. Sehemu moja tunajaribu hata kuotesha minazi. Minazi hiyo na miti yote mingine iliyopo na itakayooteshwa itasaidia kuzuia uharibifu wa ardhi. Kwa hiyo tunaomba maombi yako, ili miti hiyo iwe baraka kwa nchi hii na watu wake.

Previous
Previous

Eneo la kuku

Next
Next

Bustani yetu ya kuoteshea miti