Eneo la kuku

Chicken coop.jpg

Tumejenga eneo jipya kwa ajili ya kuku wetu. Kwa jumla eneo hilo lina 1.500 mita mraba, na tutafuga kuku humo kwa njia endelevu. Tumezungushia eneo hilo na fensi mbili, moja ya vitobo vikubwa na nyingine fupi yenye vitobo vidogo. Fensi hizo tumechimbia chini kama sentimita kumi hivi. Hivyo wanyama wakali watashindwa kujiingiza kwa urahisi, lakini pia vifaranga watashindwa kutoka. Tulianza kufuga kuku mpaka tukafikia 24 kwenye fensi nne ndogo. Lakini mbinu hii siyo endelevu, na kwenye eneo jipya tunaweza kufuga kuku hadi 250 kwa njia endelevu. Kuku watakuwa na eneo la kutosha kutembea na kukwangua. Hatua itakayofuata ni kupanda miti inayoota haraka na kuzaa matunda, ili kuku wapate mazingira wanayoyapenda.

Previous
Previous

Wageni wa Jumapili ya Pasaka

Next
Next

Kupanua eneo la bustani ya miti