Bustani yetu ya kuoteshea miti

JPEG image-CC6034CD7F74-1.jpg

Mwezi wa kumi mwaka wa 2017 nilisafiri Afrika mara ya kwanza katika maisha yangu, ili niwatembelee Alice na Martin Tlustos huko Tanzania. Nilipofika kwenye eneo la Care of Creation, Alice alitoa wazo la kwamba labda ingesaidia kuanzisha bustani ya kuotesha miti. Kwa hiyo nikaanza kuchora ramani ya mpangilio. Eneo ambalo lilipangiwa kuwa na bustani ile lilikuwa kavu na lenye miba ya mita mbili kwenda juu. Ilikuwa kazi ngumu kuamini kwamba hapa pangeweza kuwa na bustani yenye miche mingi midogo ingewezekana.

Mwaka mmoja baadaye, nikasafiri tena kwenda Tanzania, ila mara hii nikakaa kwa miezi mitatu ili nianzishe bustani kwelikweli. Kwa kweli sikuwa na furaha nilipopanda ndege kule Austria. Eneo ambalo nilikoelekea lilikuwa la joto, na haikuonekana nzuri zaidi sana kuliko wakati nilipoenda mara ya kwanza.

Lakini katika miezi hiyo mitatu sikuanza kujenga ile bustani ya miti tu, lakini pia Mungu aliniita kwenye msonge kumtumikia Tanzania na kuendeleza ile bustani ya kuoteshea miti. Nilivutana sana na Mungu, nikajadiliana na Mungu nikijaribu kumpinga mpango wake. Sikutaka kwenda Afrika tena. Lakini, mwanzoni mwa mwaka wa 2020 nikasafiri tena Tanzania kama missionali na kuanza kuendeleza bustani ile. Saa hizi, baada ya mwaka mmoja, pamoja na tukio la kuumwa na mbwa mwenye kichaa na kupewa chanjo za dharula, na baada ya kupata ajali ya kuteguka mguu wangu na kulala usiku mmoja kwenye hospitali, Mungu alibadilisha moyo wangu. Upendo ule Bwana Yesu alio nao kwa watu wa Tanzania, aliniwekea na moyoni mwangu. Nilihitaji tu kukubali kushughulika na kazi Mungu aliyonipa. Mpaka sasa, tumeshaotesha zaidi ya miche elfu nane, tumenunua tenki ya maji kwa ajili ya kuimwagilia miche, na kupanda miti ya kivuli kwa ajili ya miche midogo. Na Mungu ananifanikisha katika kazi hiyo, pamoja na kunipa furaha na upendo kwa wenyeji wa hapa. Tayari natazamia mbele nipate kuona ni nini Mungu alichonipangia mbele!

Previous
Previous

Kupanua eneo la bustani ya miti

Next
Next

Tovuti