Chanzi
Chanzi ni aina ya nzi mwenye faida kwenye shamba letu. Takataka ya jikoni na matunda yaliyooza yanaliwa na funza wao, na hao ndio tunawalisha samaki na kuku wetu. Unaposikia neno “nzi” kawaida utafikiria wale nzi wasumbufu wanaoshambulia vyakula na kusumbua kwenye vyoo na kusambaza magonjwa ya matumbo. Lakini chanzi ni tofauti. Funza tu wanakula,
lakini nzi wenyewe hawali. Kwa hiyo hawawezi kusambaza magonjwa na hawana hatari kwa binadamu.