Ushuhuda wa Martin

Kwa kadiri ninavyoweza kukumbuka, nimekuwa nikivutiwa na mambo ya mazingira kila wakati. Nilifurahia kuzunguka-zunguka peke yangu msituni na kuwatazama sungusungu wakitengeneza makaazi yao. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu kuu iliyonifanya niingie kwenye elimu ya kuwa mtaalamu wa misitu. Katika darasa la nne la shule ya misitu, nilikutana na Yesu na kubadilishwa maisha yangu. Wakati nilipokutana naye kibinafsi, ilikuwa wazi kwangu: ndivyo ninataka kufanya kwa maisha yangu yote! (Ingawa sikujua wakati huo hii ilimaanisha nini haswa).

Tangu wakati huo, hizi "nyuzi nyekundu" zimeambatana nami katika maisha yangu: Kwa upande mmoja, upendo na shauku kwa ajili ya ujumbe wa ajabu wa upendo wa Mungu unaotufikia katika Yesu Kristo; kwa upande mwingine, shauku na maslahi katika kila kitu kinachohusiana na asili.

Kwa bahati mbaya, katika ulimwengu wa madhehebu ya wokovu (nyumba yangu ya kiroho), wazo la utunzaji wa uumbaji linachukuliwa tu kama "kumbukumbu ya mbali", kwa hivyo nyuzi hizi mbili nyekundu katika maisha yangu hazikuunganishwa kwa miaka mingi.
Kisha mwaka wa 2014 tulikutana na Ed Brown, kiongozi wa "Care of Creation" kule Marekani, mojawapo ya mashirika machache ya kiinjili yanayoshughulika na utunzaji wa uumbaji. Kwanza kupitia kwake (na kisha kupitia mafunzo ya Biblia), nilitambua kwamba utunzaji wa uumbaji ni mada yenye umuhimu katika Biblia, na pia mojawapo ya matokeo yenye mantiki ya utu wa Mungu.

Kupitia kwa rafiki kutoka Tanzania, ndipo tulipokutana na uongozi wa Kanisa Anglikana, ambao walikuwa wakiomba kwa miaka kadhaa ili kupata wafanyakazi kwa ajili ya huduma ya utunzaji endelevu wa kilimo na uumbaji. Wao walikuwa na zaidi ya heka sitini za ardhi isiyotumika pamoja na kituo cha mafunzo chenye vyumba vya wageni, na sisi tulikuwa na maono ya kujenga kituo cha mafunzo kwa kilimo endelevu. Hapo wamekutana watu walio na lengo moja! Kwa hiyo sasa, tangu 2017, tumekuwa hapa karibu na Dodoma na pamoja na wafanyakazi wetu wa shambani na wenzetu katika Kanisa Anglikana, tunapata kujenga eneo hili kwa njia ya kumtukuza Mungu, kufanya upendo wake uonekane, na kuleta matumaini kwa mavuno bora zaidi kwa wakulima wadogo wa Tanzania. Kila siku ninapotembea kwenye eneo hilo, ninajazwa upya na furaha ya huduma hii - na wakati huo huo na hali ya unyenyekevu. Msemo wangu mkuu nii huu: "Kazi nyingi, muda mfupi, nguvu ndogo, pesa chache - lakini Mungu yupo!". Kwa hiyo, ingawa kuna changamoto nyingi za kutosha, tunasonga mbele kwa shangwe kwa sababu tunajua kwamba Mungu wetu mkuu yuko pamoja nasi!
Previous
Previous

Chanzi

Next
Next

Mabwawa