Kupima mwinuko

Tunapenda kuendeleza eneo jipya, na kwa kazi hiyo ni muhimu kujiandaa vizuri. Kwa wakati huu, ujuzi kuhusu mteremko wa eneo jipya unahitajika. Hapo tutahitaji pimamaji ya kamba, fimbo mbili na watu watatu. Tunafunga kamba ya mita kumi hivi kwenye fimbo hizo mbili. Ni muhimu kamba ifungwe kwenye urefu uleule! Halafu mtu mmoja anshika fimbo ikae wima upande mmoja wa shamba. Mtu wa pili anaingia shambani mpaka kamba inapata mvuto mzuri. Mtu wa tatu anaweka pimamaji katikati ya kamba na kuangalia mwelekeo. Halafu yule mtu ambaye anashika fimbo ya pili anahitaji kuhamisha fimbo kwenda juu au chini, kufuatana na maelekezo ya mtu kwenye pimamaji. Zoezi hilo linafanywa mpaka pimamaji inaonyesha usawa wa kamba. Halafu tunapiga mambo kwenye fimbo ile ya pili. Yule mtu ambaye anashika fimbo ya kwanza anaendelea mbele tena mpaka kamba inapata mvuto tena, na tunatafuta tena usawa wa mwinuko. Zoezi hili tunarudia hadi tumevuka eneo lote. Halafu tunashuka chini mita kama 30 hivi na kurudia zoezi tena.
Mwishoni tunaingiza vipimo vyote kwenye simu ya mkononi tukitumia app ya vipimo iliyo bure. Kwa njia hiyo hatuhitaji hata vifaa vya gharama kubwa kwa uchunguzi, ni rahisi sana.
Previous
Previous

Faida isiyotarajiwa

Next
Next

Chanzi