Ni baraka ya kipekee kuweza kufurahia kondoo 65 mbalimbali. Jana jioni,
niliamua kuwatembelea tena. Nilichukua majani mabichi na kutupa majani juu
ya fensi kwenye eneo la kondoo. Tunao kondoo wengi wa asili, ambao ni
wadogo, wana nguvu sana na wanavumilia vitu vingi bila tatizo lolote. Wote
walijaribu wapate sehemu yao ya majani. Kondoo wetu wawili wa "Dorper", ambao ni wakubwa zaidi kuliko kondoo wa Kiafrika, walikuja pole pole, wakakaribia eneo ambalo majani yalikuwa yameanguka. Kwa tabia ya upole sana na ,walipata sehemu yao. Hawakupigana, au kuruka au kusukuma wengine. Kwa tabia yao ya upole walikwenda tu mahali walipotaka kwenda. Nilishangazwa na ukweli ya kwamba kondoo hawa wawili wangeweza kutawala eneo lote na wangeweza kuwalazimisha wengine wote kwenda mahali walipotaka waende, lakini walikuwa wapole, wastaarabu, walitembea kwa usalama kabisa. Waliwaheshimu wengine ambao wana tabia tofauti. Nilidhani kwa sekunde kwamba kondoo hawa hawana akili, lakini hapana, walionekana kuwa na akili sana, wapole tu na watulivu. Wakati nimesimama hapo na kuwatazama kondoo, mmoja wa wachungaji alikuja kujiunga nami. Alipokaribia yule mchungaji, kondoo mmoja wa kienyeji, kondoo mweupe mdogo wa jike alikimbia kuelekea kwenye uzio na akaruka kusimama kwa miguu miwili kuwa karibu na mchungaji. Wakati huo huo mchungaji alimpapasa kondoo na akasema: “Huyu ni rafiki yangu wa karibu.” Inashangaza sana kwamba hata kondoo anajua hii.