Care of creation ni huduma ambayo ina utaratibu na muongozo kwa ajili ya wafanyakazi wake na utaratibu wa kila siku kwa wafanyakazi kuanzia jumatatu mpaka ijumaa. Kila mfanyakazi anafika kazini kwa kuzingatia sana muda. Muda wa kazi huwa inaanza saa mmoja kamili mpaka saa kumi na mmoja na nusu na kila siku ya kazi kuna mdaa wa mapumziko ya asubuhi na mchana kwa wafanyakazi wote. Kila siku kabla ya kuanza kazi tunamtanguliza Mungu kwa maombi na baada ya kazi tunafunga kwa maombi ya shukulani . Utaratibu wa kila siku baada ya maombi kila mfanyakazi anachukua vitendea kazi kwa kulingana na kazi ya eneo lake na kwenda kwenye eneo lake la kazi mpaka saa tatu na nusu. Hapo tunakuwa na mapumziko tukipata chai kwa pamoja mpaka saa nne kamili, halafu tunakuwa na kipindi cha kutafakari Biblia na kumwimbia Bwana. Tunaulizana maswali na tunakusanya maombi yetu na kuombeana. Baada ya hapo tunarudi tena kazi mpaka saa sita na nusu, ambapo tunapata mapumziko ya mchana kwa ajili ya kila mfanyakazi akapate chakula nyumbani kwake. Saa tisa kamili tunarudi kazini tena na tunafanya kazi mpaka saa kumi na mmoja na nusu jioni na tunafunga kwa maombi. Baada ya hapo wafanyakazi wanarudi nyumbani.