Kuchunga kondoo

Bwana ndiye mchungaji wangu - kwa hiyo sisi ni wanakondoo wake. Lakini inamaanisha nini kuwa mchungaji? Ninapambana na swali hilo kila jumamosi asubuhi, kwa sababu tangu mwezi wa tisa ninasaidia kuchunga kondoo kwenye shamba letu.

Kuchunga kondoo ni kazi ngumu kuliko nilivyowaza kwanza. Mwanzoni kondoo wanakukimbia, kwa sababu hawakujui. Kupiga mlusi haisaidii, kutumia fimbo haisaidii. Kuwakimbiza nako haisaidii, kwa sababu mchungaji akianza kukimbia, na kondoo wanaanza kukimbia. Bahati nzuri hiyo shida inajitatua baada ya muda.

Kitu kimoja nilichokiona baada ya muda mfupi ilikuwa ya kwamba mimi kama mchungaji ninaona maeneo yenye malisho mazuri yaliyo mbele ya kondoo. Lakini kuwafikisha kule mara nyingine ni kazi ngumu kidogo. Kondoo wanapendelea kusimama pale kwenye malisho wanayoyaona wenyewe, hata kama malisho siyo mazuri. Hii mara nyingine inaweza kumkatisha mchungaji tamaa, kwa sababu mimi nigependa kuwafikisha kwenye malisho bora, lakini hao hawanikubali uamuzi wangu.

Kuwachunga wale kondoo kumenisaidia pia kuelewa Mungu na neno lake.

Na mimi ninahitaji kujifunza kumsikiliza sauti yake Mungu na kumfuata. Ninapomwamini Mchungaji wangu na kumkubali kuniongoza, yeye atanifikisha kwenye malisho bora. Lakini nikisimama kwa ajili kula zile rundo tatu za nyasi kavu, nitakosa yale malisho bora Mchungaji wangu aliyonipangia tangu awali. Yeye anaona mambo yote na kunijalia kila kitu. Mara nyingine njia kwenda kwenye malisho mabichi inapita porini, ambapo kuna miba kulia na kushoto. Hapo nitahitaji zaidi kumwamini na kusikiliza sauti yake anayenitangulia. Kwa sababu Yeye ndiye Mchungaji mwema ambaye anapenda kondoo zake!

Previous
Previous

Kushuka

Next
Next

Useremala