Useremala
Fenicha yetu yote (au karibu yote) ni fenicha iliyotengenezwa na fundi seremala hapa hapa Tanzania. Kila fenicha imetengenzwa na upendo mwingi na jitihada kubwa. Fenicha zinginge zimetengenzwa na Watanzania na Waaustria wakiwa wanafanya kazi hii kwa pamoja. Ukiangalia kila pisi ya fenicha inaonyeshwa uotaji wa mti uliokuwa mwanzo wake. Pia utaona michoro ya uumbaji kwenye mbao za fenicha yetu. Hakuna kinachofanana au kilichotoka kama disayni ya fenicha nyingi. Tunakumbushwa ya kwamba kila mmoja amependwa kwa sababu ni wa kipekee sana na hamna binadamu ambaye anamfanana mwenzake mia kwa mia. Ninapoandika haya ninaona viti vinne vya ofisi vinanizunguka. Vimetengenezwa kwenye bara lingine na vimesafirishwa kutoka mbali kabisa. Ninashukuru kwamba vinanisaidia kutokuumiza mgongo wangu nikiwa nakaa ofisini. Pisi moja ambayo ninaipenda zaidi ni mlango wa ofisi yangu. Ina mchoro mzuri sana wa mti na pia inaonesha kazi za upendo wa yule fundi aliyeutengeneza. Ningefurahi sana kwamba tungekuwa na vitu vichache lakini bora vinavyotukumbusha kwamba uumbaji ina thamani kubwa sana.