Pigo kubwa
Kitu cha kusikitisha sana kimetokea. Emil, ngamia wetu dume, amefariki.
Kwa sababu ya ukame, tulikuwa tukitafuta mbadala wa chakula cha mifugo yetu kila wakati. Tuliona kwamba ngamia wetu pia walikula aina fulani za mti wa maziwa (Euphorbia), ambazo zina sumu. Kwa hiyo tuliongeza Euphorbia kidogo kwenye chakula chao.
Siku moja, mti mkubwa wa Euphorbia ulikatwa. Katika jitihada za kupata chakula zaidi cha ngamia wetu, mmoja wa wafanyakazi wetu aliomba matawi madogo na kuyapeleka kwenye banda la ngamia wetu.
Kwa sababu ya ukame (na kwa sababu yeye ni dume lenye ubabe), Emil hakumruhusu Camilla kula matawi yoyote ya Euphorbia, akala yote mwenyewe. Kwa bahati mbaya, alikula kupita kiasi na sumu kwenye matawi hayo ilizuia chakula kusagwa tumboni, hivyo baada ya siku chache akafariki.
Tunasikitika sana kwa hili. Hatujapoteza mnyama tu, bali pia sehemu ya thamani ya timu wetu. Hasa Camilla amehuzunika sana. Ngamia ni wanyama wa kijamii, na kumwacha peke yake kutamsababishia msongo mkubwa wa mawazo. Hivyo tafadhali tuombee ili tupate fedha za kutosha za kununua ngamia mwingine haraka, ili naye asife kwa uweke pekee.