
Hongera
kwa kujisajili kwa Semina ya Huduma ya Uumbaji Tanzania!
Tumepokea maombi yako na tunatarajia sana kukukaribisha. Kukamilisha kujiandikisha kwako, tunaomba ukaweke malipo ya semina kwenye akaunti ifuatayo na usisahau kutuambia jina lako, wakati wa kulipa malipo ya semina:
Benki: CRDB PLC
Tawi: Tawi la Dodoma
Jina la Account: ACT COC TZ
BIC: CORUTZTZ
Anwani: Kuu Street, P.O.BOX 401, Dodoma
Nambari ya Akaunti ya Benki:
Akaunti ya USD: 0250286209500
Akaunti ya TZS: 0150286209500
Baada ya kulipa malipo ya semina maombi yako yamekamilika.
Tunapenda uje ya kwamba bila malipo huwezi kuhudhuria semina zetu.
Mambo yafuatayo ni muhimu kwako:
Semina hiyo inaanza Jumanne saa 6 mchana (ikiwa unawasili kutoka mbali, ni bora uwahi kufika siku moja kabla ya semina kuanza. Usisite kutuambia mipango na mahitaji yako!)
Semina hiyo itaisha Ijumaa saa sita mchana (ikiwa unakuja kutoka mbali, labda itakusaidia kuchelewa kuondoka na kupanga safari ya kurudi nyumbani kwa Jumamosi.) Tafadhali usisite kutuambia mipango na mahitaji yako!
MUHIMU: Unapaswa kuhudhuria masomo yote ya semina (simu ya mkononi hairuhusiwi wakati wa masomo ya semina) ili upate cheti mwishoni mwa semina (Jumanne saa 6 mchana hadi Ijumaa saa 6 mchana). Ratiba ya kawaida ya kufundisha ni saa 2:00 asubuhi hadi 3:00 usiku. Kwa hivyo tafadhali hakikisha kuwa huna mpango mingine wakati wa siku hizi tatu za mafunzo mazuri sana. Wakati wa breki bila shaka, uko huru kutumia vifaa vyako vya mawasiliano kama simu nk..
Ikiwa una mahitaji yoyote maalum ya chakula, tafadhali tuambie mapema.
Mahali pa Semina: Semina hiyo hufanyika Vikonje, ambako ni kilomita 30 kutoka katikati mwa jiji la Dodoma kwenye barabara ya kuelekea Morogoro. Ukifika kibao cha Vikonje, fuata barabara ya kwanza inayoenda kushoto ukipita soko la kijiji, pita kushoto na uingie barabara inayo elekea kwenye "Chuo cha Ualimu cha Kanisa Anglikana Tanzania". Mara tu unapopita geti, pita kulia na uulize hosteli ya chuo iko wapi.
Kwa maswali zaidi usisite kumpigia simu karani wetu: Shedrack Hwaiti: +255 626 312 314 (Kiswahili) au Alice Tlustos +255 623 967 220 (Kiingereza au Kijerumani)
Ikiwa una mahitaji maalum, kama vile,upo na mtoto mdogo n.k tafadhali tuambie bila kusita.
Asante sana kwa kutuamini na kwa utayari wako wa kuja kufurahia masomo ya kipeke sana!