
Permaculture
Permaculture ni mkusanyiko wa mbinu mbalimbali za maisha endelevu ambazo zinaongozwa na maadili matatu:
Kutunza mazingira
Kumjali mwenzako
Kujali vizazi vijavyo
Permaculture kama mfumo ilianzishwa na Bw. Bill Mollison katika miaka ya themanini. Inaunganisha mafundisho ya kilimo endelevu, kusimamia na kutunza maji ya mvua, kuhifadhi mazingira, kutengeneza umeme kwa njia endelevu, kuimarisha jamii na uchumi kwa njia endelevu na kadhalika.
Mbinu zote kwa jumla zinajaribu kutekeleza malengo yafuatayo:
Punguza matumizi ya rasilimali
Tumia rasilimali ileile mara nyingi iwezekanavyo
Tengeneza badala ya kununua tena
Tafuta matumizi mapya kwa rasilimali badala ya kuichoma au kutupa tu.
Kwenye shamba letu tunatumia na kufundisha mbinu mbalimbali za permaculture ambazo zinalingana na imani yetu kwa Mwenyezi Mungu. kwa mfano:
Mifereji ya kukingia maji ya mvua
Choo cha kutengenezea mboji
Mfumo wa “aquaponics” (kufuga samaki pamoja na kuotesha mboga)
Kilimo cha mseto
Ufugaji endelevu
n.k.