
Kilimo kwa Njia ya Mungu
Bara la Afrika lina maliasili nyingi kuliko mabara yote duniani. Afrika ina madini mengi sana, mawe ya thamani, na akiba za mafuta ghafi, uwezo mkubwa wa kilimo, ina watu wa ajabu, maji mengi na mito mizuri, wanyama pori wa aina mbalimbali na mimea tofauti zilizo na uwezo mkubwa wa utalii.
Kinyume na uwezo wake, Afrika ndilo bara maskini zaidi ulimwenguni, na watu wake wanaishi maisha duni, hali za ukame na shida nyingi za lishe, vifo vingi vya kutisha vya watoto wachanga, maradhi, vita, utegemezi, elimu duni, uharibifu wa misitu, ufisadi na kushuka kwa thamani za sarafu yote haya vikiwakilisha sura ya bara hili.
Wakulima wa kujimudu, wanakadiriwa kufikia asilimia themanini na tano [85%] ya idadi ya Waafrika wote, ambao wanaishi kwa matatizo ya lishe na maisha duni. Kiasi cha mazao kinachozalishwa na wakulima hawa hakitoshelezi mahitaji ya familia zao, hali inayolazimisha kuingiza mamilioni ya tani za nafaka kutoka nje kila mwaka.
Kilimo kwa njia ya Mungu ni suluhisho la ajabu la kiungu kwa tatizo la uhaba wa chakula umasikini kwa watu maskini wanaoishi vijijini. Kilimo kwa njia ya Mungu si maarifa ya teknolojia tu, lakini ni suluhisho lenye uwiano bora wa kibiblia, usimamizi na maarifa ya teknolojia kwenye miliki za kilimo, linalowawezesha masikini kujiweka huru na umasikini kwa kutumia kile ambacho Mungu amekiweka mikononi mwao na pia kuwafunulia ahadi ya uzima tele.
Kutokana na mabadiliko ya moyo katika Yesu yanatokea mabadiliko ya akili zetu katika usimamizi bora na kisha matekelezo katika kufanya kazi ili kukombolewa kwa ardhi za mashamba.
Kilimo kwa njia ya Mungu kuna sifa za mafanikio zilizohakikishwa tangu mwaka 1984, ambapo Brian Oldreive alikuwa wa kwanza katika utekelezaji wa mbinu hizo katika shamba la Hinton nchini Zimbabwe kwa kiasi kikubwa cha kibiashara, hatimaye walifikisha hekta 3500 za mimea shambani.
Tangu siku hizo za mwanzo, kilimo kwa njia ya Mungu kimeenea katika nchi nyingi, kikitumiwa na makanisa, wamisionari, na asasi/taasisi zisizo za kiserikali kote barani Afrika. Kufikia sasa, katika mwaka wa 2009, kilimo kwa njia ya Mungu imeendelea kuenea katika nchi nyingi kama, Angola, Benin, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo [DRC], Kenya, Lesotho, Madagaska, Malawi, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Siera Leone, Afrika Kusini, Swaziland, Tanzania, Uganda, Zambia, Zimbabwe na nchi nyinginezo kwa ngazi tofauti katika bara la Afrika na pia zimesambaa ndani ya nchi zingine nje ya Afrika kama Mexico, Nepali, Guyana, Umarekani, Uingereza na nyinginezo.
Kulima kwa njia ya Mungu ni kipawa kinachotolewa bure kwa mwili wa Kristo na ni mtandao wa watu walio na mioyo sawa ya kuwafikiria watu masikini na usio wa dhehebu au shirika lolote. Hadhi, uendeshaji na mipango ya kilimo kwa njia ya Mungu zinaelekezwa na timu ya waandazi mashuhuri wa kujitolea walio wakufunzi wenye uzoefu mkubwa.