Tour ya pili ya kiroho! Kwenye mashamba yetu ya maonyesho

Jumapili iliyopita tumefurahi sana kuwakaribisha wanakwaya wa kwaya ya “Tumaini” kutoka St. Luke/ Vikonje kwenye mashamba yetu ya maonyesho. Naomba ukawasikilize wenyewe wanasemaje baadaya kubarikiwa na tour yetu:
“Nawashukuru sana kwa utajiri huu. Kwa kweli nimefurahi sana na kuona kuwa, kumbe, mbinu inatuwezesha kubadili Dodoma yetu kuwa kijani kwa kutumia njia ya Mungu. Ombi langu niwaombe mzidi kutoa semina kwa jamii inayowazunguka.Kwa maana wahenge wanasema ‘mmulika nzoka wanzinzaje hamagulu’- Ili iwe mfano kwa jamii iliyo karibu nawe. Asanteni. Mungu awabariki sana katika shamba la Bwana!” (Joseph L. Chibada) “Tour au Semina ilikuwa nzuri sana. Ningependa mngeissaidia jamii inayowazunguka wafanye kama ninyi mfanyavyo kwenye mazingiria yao na mfuatilie kama kweli wanaelimika. Asanteni sana. Mbarikiwe. (Anna George Shagama) “Mimi nimefurahi sana kuona vitu vingi viilivyo hapa mitiya matunda, maua mazuri nimebarikiwa sana. Mungu awape nguvu zaidi ili mfanye aidi na bustani ipendeze zaidi pia niemfurahia kwa keki nzuri na soda. Mungu awabariki sana.” (Selina Mwaluko) “Nimependa kilimo. Semina ni nzuri sana kutokana na kilimo chenu Mungu awabariki sana!” (Suzy d. Njani) “Semina ilikuwa nzuri nimefarijika sana nayo. Nimejifunza ya kuwa katika umbaji wa Mungu inatupasa tuingie na kuiga mfano wa Mungu. Tutunze mazingira pamoja na kupanda miti, vile vile nilijifunza kuhusu kilimo kwa njia ya Mungu. Kilimo kwa njia ya Mungu kunda faida kubwa yatupasa tuingie.” (Olivia Paul Stone

Previous
Previous

Kondoo na mimi

Next
Next

Tour ya Kiroho