Ndugu wetu mpendwa sana anasherekea mbinguni sasa

Wiki mbili zilizopita tulipata ujumbe mgumu sana ya kwamba mpendwa wetu saana mfanyakazi wetu ameenda kukaa na Yesu. Oh, alikuwa ni baraka kubwa sana kwa huduma yetu!

Miaka mitano iliyopita Mzee Mgaya alijiunga na huduma yetu. Wakati huo alikuwa na maumivu makali sana kwenye miguu kutokana na ajali mbaya sana. Pia miguu na tumbo yake yalikuwa yamejaa na maji.

Wakati huo alikuwa hana tumaini kwa mwili wake na pia kwa nchi yake akikoishi. Nakumbuka tulipokuwa tunapanda karanga akapita pale, akiwa anacheka na kusema ya kwamba hapa kuwezi kupanda karanga hata siku moja. Alipoona ya kwamba baadaye tulivuna vizuri saaana akashangaa na kutaka kabisa naye ajifunze mbinu ya Kilimo kwa Njia ya Mungu. Alikuwa ni balozi na alipenda sana watu wapate kusaidiwa kwa mbinu hiyo. Tukamwajili na akiwa ni mlinzi mzuri sana kwa miaka miwili, baadaye akawa mtunza bustani kwa mwaka moja. Tulipoona ya kwamba kondoo wetu wanampenda kuliko watu wote, tukamwomba awe mchungaji wa kondoo wetu (miaka miwili tena). Mwanzoni wa huduma yetu akapata kumfahamu Yesu na akamkaribisha moyoni. Kutoka pale alipenda sana kuimba wimbo moja unaoenda hivi,” Amani moyoni mwangu, kwa Yesu Mwokozi wangu, sina shaka kamwe, kwa sababu Yeye, yu nami moyoni mwangu!” Alilala kwa amani, Yesu alipokuja kuchukua mkono wake na kumkaribisha mbinguni. Sisi, kama team ya watu wa Care of Creation Tanzania, tunasikitika sana, maana tunammiss kila siku. Lakinin tuna uhakika ya kwamba amepata amani kweli kweli sasa. Kwa upendo mkubwa sana kwake, tunawaombea familia yake ili wabarikiwe sana na Bwana akavute machozi yao yote.
Previous
Previous

Miti malisho

Next
Next

Ulinzi endelevu wa mimea