Choo cha shambani

Katika miezi iliyopita mimi, Felix, nimeunda na kujenga choo cha shambani. Lengo la huduma hii ilikuwa ni kujenga vyoo vingi zaidi vilivyosambazwa shambani, ili njia za kwenda chooni ziwe fupi na wafanyakazi na wageni wasilazimike kwenda kwenye choo chetu kikubwa cha mbali kidogo. Kama ilivyo
kwa choo chetu kingine, maji hayatumiwi, lakini kinyesi hukusanywa kwenye ndoo na kufunikwa na unga wa mbao. Kwa njia hii haina harufu na baada ya miezi minne hadi sita ya kuozeka inaweza kutumika kama mbolea. Choo kina msingi wa saruji ambamo ndoo iko. Kupitia ngazi chache kupandia juu kuna kachumba kadogo, ambayo iko juu yake. Hii inafunikwa pande zote na bodi za mbao. Kwa ulinzi wa mvua na jua kuna paa rahisi ya bati juu yake.
Baada ya kumaliza kubuni na kuchora ramani, tulianza kujenga choo cha kwanza. Kwanza tuliagiza fremu ya chuma, ambayo mbao na paa zingewekwa, kutoka kwa fundi. Baada ya wiki moja ilikuwa tayari. Nikiwa na kazi ya kutoboa vitobo kwa ajili ya boliti, fundi alianza kuweka msingi na kujenga
chumba cha chini cha ndoo. Kwa pamoja tukaweka kiunzi na kumaliza muundo mdogo pamoja. Katika mchakato huo, tulikuwa na wakati mzuri, furaha nyingi, na kuwasiliana vizuri licha ya changamoto ya lugha tofauti. Jengo na urekebishaji wa paa la bati lilikuwa gumu zaidi na la kusumbua kuliko nilivyofikiria, lakini mwishowe ilifanika vizuri. Hatua ya mwisho ilikuwa kuandaa na kuweka mbao. Tulinunua mbao katika kijiji cha jirani. Nikiwa na mwenzangu Noah nilizikata kwa saizi, nikatoboa mashimo kisha nikazifunga kwenye fremu ya chuma kwa boliti. Kisha mfanyakazi alipaka mbao kwa varnish yenye rangi nyekundu na hivyo kukamilisha choo. Hata kama sio kila kitu kilienda kama ilivyopangwa, kulikuwa na shida na usumbufu, choo cha kwanza bado ni mafanikio kabisa na katika siku zijazo labda kutakuwa na vingine kwenye shamba letu...
Previous
Previous

Mlonge

Next
Next

Mahusiano ya kufaidiana