Sherehe ya Krisimasi

Mwaka huu sherehe ya Krismasi ya Care of Creation Tanzania ilikuwa ya kipekee sana. Tulipata zawadi nzuri sana ya wafadhili nje ya nchi wengi, wenye upendo, ili tuweze kuwa na chakula kizuri wa Krismasi, kama pilau, keki, matunda, soda baridi na kila mfanyakazi alipata bahasha nzuri yenye zawadi, kwa ajili ya chakula cha sherehe ya Krismasi kwa ajili ya familia yake yote. Asante sana Mungu, asanteni sana wapendwa wafadhili wetu! Kusherekea Tanzania ina maana ya kwamba,utavaa nguo nzuri, kula chakula kizuri na kucheza. Pia tulikuwa na wakati mzuri sana wa kutafakali tunaweza kushukuru kwa ajili ya nini, kilichotokea mwaka uliopita. Kulikuwa na mengi ya kushukuru. Furaha ilijaa kwenye ukumbi wetu, kweli kweli. Mwishoni picha ya sherehe ya Krismasi ilipigwa na la ajabu,- sisi ni zaidi ya watu 40 kama wafanyakazi katika huduma ya Care of Creation Tanzania sasa. Mungu asifiwe sana!

Previous
Previous

Mbuyu

Next
Next

Kondoo na mimi