Chakula cha kuku
Kama binadamu wanavyohitaji kula vyakula mbalimbali vyenye lishe bora, vilevile na kuku wanahitaji malisho bora yenye lishe mbalimbali. Sehemu moja muhimu ni vyakula vyenye nafaka na proteini, kwa mfano mahindi, nafaka nyingine, jamii ya maharage n.k. Ni muhimu pia kuchanganya vyakula hivi kwa uwiano unaofaa. Uwiano kati ya proteini na proteini na hamirojo iwa kati ya 1:3 - 1:9, ili kuku wasinenepe mno wala wasipate upungufu wa malisho na kuathirika mwilini kama kwa mfano shida kwenye figo. Lishe nyingine yenye umuhimu ni minerali. Kalisi inahitajika kwa ajili ya kupata maganda ya mayai yenye nguvu, na pia kwa ajili ya kuimarisha manyoya. Ili uongeze kalisi kwenye chakula cha kuku unaweza aidha kuponda maganda ya mayai na kuchanganya na vyakula vingine, au unaweza kununua dukani. Kwenye shamba letu tunajitahidi kuboresha maisha ya kuku wetu siku hadi siku.