Tunapenda kujivunia kusema kwamba kwenye shamba letu, kuna idadi kubwa zaidi ya ndege kuliko sehemu yoyote nyingine hapa karibuni. Mwaka 2017, tulianza kuleta tena mazingira yenye afya katika eneo lenye ukame nchini Tanzania na kupanda maelfu ya miti. Hivyo, tumeweza kuunda mazingira bora kwa wanyama wengi, ikiwa ni pamoja na ndege wengi.
Tangu wakati huo, idadi ya ndege kwenye shamba letu imeendelea kuongezeka.
Martin alianza kutembea mara kwa mara kwenye shamba letu na kudokumenti ndege wanaoishi. Kwa sasa, kuna zaidi ya aina 50 tofauti ambazo anaweza kuzirekodi kwa mara kwa mara. Jumla ameweza kurikodi zaidi ya aina 100 za ndege kwenye heka 60 hivi. Bara yote ya Ulaya ina aina kama mia nne na kidogo… ;-)
Wakati Martin na Alice walienda Ulaya (Novemba 2023 hadi Januari 2024), ikawa zamu yangu (Dominik) kutumia muda mara moja kwa wiki kuangalia marafiki wetu wa angani na kuhakikisha kuwa hakuna pengo la data wakati Martin hayupo.
Kila wakati ninapoangalia, naona ndege za kila aina na rangi. Kutoka kwa manyoya yanayong´aa ya zambarau na buluu, hadi kijani na njano na hata nyekundu, kila rangi inawakilishwa kwenye manyoya ya aina mbalimbali.
Na pia, sauti na makelele ya wakazi wa angani yanaweza kusikika kote shambani. Popote ninapoenda, nyimbo na kelele za ndege vinaniandamana.
Tuna shukrani kubwa kwamba tumeweza kuleta tena uhai mwingi kwenye shamba letu, ambapo hapo awali, viumbe wa porini walikuwa wanakaribia kutoweka, na tunatumai kuwa maendeleo haya yataendelea.